Mtandao wa Uwanja wa Siasa

Mtandao huu unazinduliwa kwa lengo la Kutoa fursa kwa Watanzania kutumia uhuru wao, haki yao ya msingi kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa kutekeleza moja ya misingi yetu ya kujenga jamii ya Watu walio sawa na huru. Lakini pia ni muhimu kuweka bayana kuwa uhuru wa Kutoa mawazo lazima uambatane na kanuni ya demokrasia na nidhamu ya kutambua kuwa kila mtu anastahili heshima ya kutambuliwa kuthaminiwa utu wake, na kwa hiyo wachangiaji katika mtandao huu watapaswa kutambua hilo ili mtandao huu usitumike kama eneo la malumbano na ama kukashifiana kati ya mtu na mtu au kikundi kimoja na kingine.

Huu ni mtanadao huru haufungamani na chama chochote cha siasa, kundi lolote la kijamii, dini, kabila, rangi, ukanda na ama Ubara na Uzanzibarii. Muhimu ni maoni yako, hulazimiki kuandika jina lako au kuandika anuani yako. Unaweza kutumia jina la utani.

Tunakusudia kutumia fursa hii kuwafanya viongozi wetu wanao shika nafasi muhimu za uongozi wa nchi yetu kupata nafasi ya kujua maoni ya Watanzania katika maeneo wanayoyaongoza. Hatuwezi kuendelea kujinyima fursa hii ya kushiriki katika uongozi wa nchi yetu. Sisi ni wadau katika Serikali yetu. Tunawajibu wa kushiriki badala ya kuwa walalamikaji na wanung’unikaji ndani ya nchi yetu, haya shime tuwe tayari kujenga nchi yetu kujenga utaifa wetu na uzalendo kwa faida yetu ya sasa na vizazi vijavyo.

MUNGU IBARIKI TANZANIA




Uwanja wa Siasa
Habari Mbalimbali